Headlines

FASHION : COBESO KUZINDUA COBESO TV KATIKA KILELE CHA MR_MISS CBE 2015

By Sebastian - Monday, April 13, 2015 No Comments
Serikali ya wanafunzi wa chuo cha elimu ya Biashara Dodoma (CBE Dom) kupitia kwa wizara ya Habari chuoni hapo, iko mbioni kuzindua kituo mtandao cha televisheni ambacho kitafahamika kama COBESO TV, uzinduzi huo wa aina yake umepangwa kufanyika katika kilele cha sherehe za Mr & Miss CBE 2015.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Sebastian Okiki, akiongea na wanahabari wetu, alisema uzinduzi huo utaenda sambamba na kuzindua mtandao wa kijamii wa chuo cha CBE maarufu kama CBE Social.

"Tumepanga kuzindua media hizi mbili kwa wakati mmoja ili kuwawezesha wanacobeso kunufaika na matunda ya elimu ya viongozi wao. Kwa kweli ni faraja kubwa sana kuwa sehemu ya mafanikio haya".. Alisema Okiki

Katika upande wake, Waziri wa Habari chuoni hapo, alitoa shukrani zake za dhati kwa wanacobeso kwa kuwa walikuwa sehemu kubwa ya mafanikio ya wizara hiyo.


-------------------------
COBESO TV


Tags:

No Comment to " FASHION : COBESO KUZINDUA COBESO TV KATIKA KILELE CHA MR_MISS CBE 2015 "